Marehemu Lucy Kibaki akiwa na Mumewe Rais Mstaafu wa Kenya Mzee Mwai Kibaki siku ya ndoa yao mwaka 1962.
********
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemtumia
salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kenya mheshimiwa Uhuru
Kenyatta,kufuatia kifo cha mke wa Rais Mstaafu wa Kenya mama Lucy
Kibaki aliyefariki dunia leo tarehe 26 April 2016
Mama
Lucy Kibaki ambaye ni mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai
Kibaki amefariki dunia jijini London nchini uingereza ambako alikuwa
akipatiwa matibabu.
Katika
salamu hizo,Rais Magufuli ameeleza kushtushwa na kifo hicho na kuongeza
kuwa Kenya imempoteza mtu mhimu aliyetoa mchango mkubwa katika
maendeleo ya nchi yake.
"Kupitia kwako Rais wa Jamhuri ya Kenya mheshimiwa Uhuru Kenyatta napenda kumpa pole nyingi Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki,Familia yake,ndugu,jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu mkubwa." Amesema Rais Magufuli.
Dkt John Pombe Magufuli pia amemuombea marehemu Lucy Kibaki apumzishwe mahali pema peponi,Amina.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,IKULU
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,IKULU
Dar es salaam
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment