Ulisikia Taarifa za HAZARD Kuhama CHELSEA? Kamwambia Hivi Kocha Mpya wa CHELSEA

Kama utakuwa unakumbuka vizuri habari za kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji anayeichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza Eden Hazard kuhusishwa kutaka kuihama klabu hiyo, April 18 2016 zimetoka stori mpya kuhusu kiungo huyo ambaye alijiunga na Chelsea akitokea Lille 2012.

April 18 2016 stori kutoka sokkaa.com wameandika kuwa Eden Hazard tayari ameongea na kocha mpya wa Chelsea Antonio Conte ambaye atajiunga na timu mwishoni mwa msimu, Hazard amemwambia Conte kuwa ataendelea kubakia katika kikosi cha Chelsea msimu ujao kama kawaida na wala hana mpango wa kuhama.

Hazard ambaye mwaka uliyopita alishinda tuzo ya mchezaji bora wa PFA na FWA alikuwa anahusishwa na kutaka kuondoka Chelsea mwishoni mwa msimu, huku vilabu vya Real Madrid na Paris Saint Germain vilikuwa vikihusishwa kwa karibu kumuhitaji, Hazard bado amebakiza mkataba wa miaka minne na Chelsea.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment