
Spika Job Ndugai.
Nasema hayo kutokana na malalamiko yaliyoanza kujitokeza kuhusu hujuma mbalimbali ambazo zimeanza kuibuliwa. Sitaki kusema ni zipi kwa sababu ni nyingi, nanyi mnazijua. Nasema hivyo nikiwasisitiza kuwa, kuanika uozo kwanza ndiyo kazi yenu ikiwa ni pamoja na kuisimamia serikali.
Mkifanya hivyo mtakuwa mnamsaidia Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kazi yake ya kutumbua majipu ambayo yameumiza taifa hili kwa kipindi kirefu sasa.
Wakati wa kampeni za urais mwaka jana, Magufuli alisema kwamba, yeye si mkali ila linapokuja suala la kuwaletea wananchi maendeleo ambayo amekuwa akisisitiza kuwa hayana itikadi za vyama, “nitakuwa mkali na dikteta wa maendeleo.”
Aliwahi kusema hivyo katika moja ya mikutano yake.
Duru kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinasema uamuzi wake wa kuchukua fomu za kukiomba chama chake kimteue kuwania urais 2015 alishawishiwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, rafiki yake wa karibu ambaye hakusita hata siku moja kumuunga mkono na kumtetea wakati alipojikuta kwenye matatizo. Hata Rais wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi alimsifu Magufuli akimtaja kuwa yeye ni simba wa kazi.
Dk. Magufuli ni mtu wa takwimu, ana kumbukumbu imara na linapokuja suala la kutoa tarakimu za kilomita au pesa, hapati shida kuzitaja kwa sauti pale anapoulizwa na waandishi wa habari au kwenye shughuli za uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara.
Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, mwaka 2010, Magufuli alitakiwa na mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete (pia wakati huo rais wa awamu ya nne) aeleze utendaji wa chama na serikali yake katika sekta ya ujenzi wa barabara.
Magufuli alijibu kwa kutaja mahsusi idadi ya barabara zinazojengwa na zilizokamilika. Hakuishia hapo, alitaja pia maeneo, yaani mikoa, wilaya na hata vijiji zinakojengwa.
Dk. Magufuli sasa anaendesha kampeni ya mabadiliko akiahidi kushughulikia tatizo la rushwa kwa kuanzisha mahakama ya wala rushwa. “Kiama cha mafisadi kimewadia.” Amekuwa akisema hayo karibu katika kila mkutano wa kampeni anaohutubia.
“Sikuomba nafasi hii kwa majaribio, niliomba kwa ajili ya kufanya kazi na kuwatumikia Watanzania. Naijua vizuri historia ya nchi hii, najua tulikotoka, tulipo sasa na tunakoelekea,” aliwahi kusema Rais Magufuli.
Ni wajibu wa wabunge sasa kuachana na tabia iliyokithiri ya kumezwa na itikadi za vyama na kutetea mafisadi kama ilivyokuwa huko nyuma. Naamini kuwa, enzi hizo za kushabikia ufisadi zimepitwa na wakati, sasa ni hapa kazi tu!
Itashangaza sana katika utawala huu wa Magufuli kuona mbunge anatetea ufisadi kwa sababu kiongozi mwenyewe ni adui wa ufisadi.
Ndugu zangu wabunge, tafadhalini sana safari hii tuachane kabisa na kushabikia ubadhirifu, wizi wa mali za umma. Yeyote anayejihusisha na mambo hayo awe adui namba moja wa nchi. Nasema hayo kutokana na ukweli kwamba ufisadi ndiyo umetufikisha hapa tulipo leo na baadhi ya wabunge walikuwa wakiutetea.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment