WAZIRI
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema hakuna
taasisi ya Serikali wala binafsi nchini iliyojenga nyumba za bei nafuu.
Kutokana
na hali hiyo, amesema Serikali imekusudia kuanzisha Sheria ya Mamlaka
ya Kuratibu Shughuli za Ujenzi, itakayodhibiti bei za nyumba nchini.
Akizungumza
jana katika mkutano na wajenzi kuhusu kusudio hilo la Serikali
kuanzisha sheria na mamlaka hiyo, Lukuvi alisema taasisi zote
zinazotumia wimbo wa nyumba za bei nafuu, hazisemi ukweli.
Alitoa
mfano wa nyumba zilizojenga na Mifuko ya hifadhi za jamii na Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na mashirika mengine binafsi na kudai ni
za gharama nafuu kwamba zinauzwa bei inayoanzisha Sh milioni 50 na
kuendelea. Alisema bei hiyo si nafuu hata kidogo kwa Watanzania walio
wengi.
Kutokana
na changamoto hiyo, Lukuvi alisema Serikali imetafuta wabunifu wa
kujenga nyumba ya bei nafuu na kupata Kituo cha Social Business,
kilichopo Babati mkoani Manyara wanaojenga nyumba ya vyumba viwili vya
kulala kwa Sh milioni 15.
“Hebu
fikiria kwa nyumba ya vyumba viwili huko Babati wanajenga kwa gharama
hiyo wakati Dar es Salaam vifaa vyote vinapopatikana wanajenga kwa Sh
milioni 50 na hapo Mtanzania wa kawaida atalipa kwa miaka 30 ya uhai
wake wote,” alisema.
Kuhusu
Sheria na Mamlaka ya Kudhibiti Ujenzi, Lukuvi alisema itakamilika mwaka
huu kwa ajili ya kulinda wamiliki, wapangaji na Serikali kukusanya
mapato yake.
Alisema
ni lazima kuwe na mfumo na sheria wa kusimamia wajenzi kwani
wanasababisha kwa kiwango kikubwa miji kutopangika huku serikali za
mitaa zikishindwa kukusanya mapato yake.
Lukuvi alisema ni lazima eneo hilo la ujenzi lisimamiwe kwani duniani kote ndiyo linalotumika kutakatisha fedha chafu.
Kuhusu
watakaoshindwa kujenga nyumba za gharama nafuu, Lukuvi alisema pia
wataweka haki za wapangaji hasa mijini kwani wanaandaa sera ya makazi na
nyumba ili mpangaji awe na sheria inayomlinda.
Alisema
kwa sasa mjenzi anapangisha nyumba kwa gharama kubwa hata kama haina
baadhi ya vitu, hivyo lazima alipe gharama kulingana na ubora wa nyumba
inayofanana na thamani ya fedha kwani wapangaji wengi wanalipa kulingana
na anachotaka mlipaji.
Alipoulizwa
kuhusu kodi kubwa kuchangia gharama za nyumba kuongezeka, Lukuvi
alisema taasisi nyingi bado hazijajishughulisha na kutafuta teknolojia
za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, badala yake zimekuwa zikilalamika
kodi za Ongezeko la Thamani (VAT) pamoja na kodi nyingine.
Alisema
kama taasisi hizo zitafuata teknolojia katika nchi zilizoendelea,
zitajenga nyumba za gharama nafuu ambazo kila Mtanzania anaweza kumudu.
“Bado
nawapa changamoto, wasilete visingizio vya kodi, watafute teknolojia
zilizopo huko duniani. Bado hakuna taasisi inayoniridhisha,” alisema.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment