Upande
wa Mashitaka katika kesi ya Josephat Gwajima, Askafu wa Mkuu wa Kanisa
la Ufufuo umekataa kuendelea kupeleka mashahidi wake katika Mahahaka ya
Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kutaka kesi isimamishwe ili isikilizwe
rufaa yao.
Upande
wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo notisi ya rufani tarehe 25
Aprili mwaka huu, kupinga kutopokelewa kwa ushahidi wao wa CD na picha
zilizopelekwa mahakamani hapo.
Shadrack
Kimaro, Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali aliiomba mahakama kuwa, kesi
hiyo isimamishwe mpaka utakapotolewa uamuzi wa rufaa ya kupinga
kukataliwa kwa ushahdi wa CD na picha zilizofikishwa mahakamani hapo
kama kielelezo cha kesi hiyo.
Shadrack
amesema kuwa, ushahidi huo ulioambatana na ripoti ya mtaalamu wa picha
na barua ya ZCO iliyokwenda kwa mtaalamu wa picha, vyote vilikataliwa
mahakamani hapo.
Hata
hivyo, upande wa mshtakiwa uliomba mahakama kufuta kesi hiyo kutokana
na upande wa mashitaka kukosa ushahidi na kwamba kesi haiwezi
kusimamishwa kutokana na kungojaa rufaa iliyokuwa bado haijafunguliwa.
Cyprian
Mkeha, Hakimu Mfawidhi baada ya kusikiliza pande zote mbili amesema
kuwa, kesi hiyo itatajwa tena tarehe 2 Juni mwaka huu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment