VIDEO: Smartphone ya Kwanza ya Robot Duniani Imeanza Kuuzwa Leo, Check Uwezo Wake Hapa


Teknolojia inazidi kukua kwa kasi na uvumbuzi wa vifaa mbalimbali vya urahisishaji wa kazi vinatengenezwa, kwa mara ya kwanza duniani simu iliyotengenezwa kama roboti imeanza kuuzwa rasmi leo May 26 2016, Simu hiyo imeitwa RoBoHon na imetengenezwa katika size kama simu nyingine isipokuwa tu muundo wake ambao ni kama binadamu ambaye anatembea na mwenye uwezo wa kucheza pia.
Simu hiyo iliyotengenezwa na kuzinduliwa huko Japan inauzwa paundi 1200 ambazo ni zaidi ya milioni 30 za kibongo . RoboHon ina uwezo wa kukusaidia kupokea simu unapokua busy na kujibu meseji kwa niaba yako na kuwa kama msaidizi wako binafsi pia inakukumbusha juu ya matukio muhimu unayopaswa kuyafanya.


Kampuni ya Sharp inasema itatengeneza simu 5000 za aina hiyo kila mwezi na inadhamiria kuwa kampuni inayoongoza katika mauzo ya simu za aina hii.
Bonyeza Play hapa chini kucheck uwezo wa simu hiyo;
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment