Waliomtukana Rais Nchini Uturuki Wafikia 2000, Mrembo wa Taifa Kahukumiwa Kwenda Jela


Hata Tanzania imeshuhudia baadhi ya watu wakipelekwa Mahakamani kwa kumtusi Rais au kuandika habari za uongo kuhusu viongozi wengine wa nchi na hii ni baada ya sheria mpya ya makosa ya mitandao kuanza kufanya kazi.

Huko Uturuki habari nyingine kubwa ni hii ya Mahakama kwenye mji wa Istanbul kumhukumu mshindi wa zamani wa shindano la urembo nchini Uturuki kwa kosa la kumtukana rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.
 
Kwa mujibu wa BBC Swahili , Merve Buyuksarac mwenye umri wa miaka 27 alipatikana na hatia ya kumtukana hadharani President wa Uturuki hivyo amehukumiwa kifungo kilichoahirishwa cha miezi 14 gerezani.

Inasemekana pia mrembo huyu aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii pamoja na kuwatumia watu shairi lenye matusi katika mtandao wake wa Instagram lakini Wakili wake amesema wamepinga hukumu hiyo katika Mahakama kuu ya bara la Ulaya na Buyuksarac amekanusha madai yote dhidi yake.

Wanaharakati wa kupigania haki za Binadamu wanasema hiyo kesi ni njia ya serikali ya rais Erdogan kukandamiza uhuru wa kujieleza ambapo hadi sasa watu 2000 wengi wao wakiwa ni Wasanii nyota na hata wanafunzi wameshtakiwa kwa kumkejeli au hata kumtusi Rais huyu tangu mwaka wa 2014.
BBC wameripoti kwamba hukumu hiyo iliahirishwa ilimradi tu asirudie makosa hayo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment