Malengo na Kauli ya Kocha wa YANGA SC, Hans van Pluijm Kuhusu MEDEAMA ya Ghana

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika klabu ya Dar es Salaam Young Africans, July 4 2016 wameendelea na mazoezi ya kuelekea mchezo wao wa tatu wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam July 15 2016.

Yanga ambao wapo Kundi A nafasi ya mwisho, kundi ambalo lina timu za TP Mazembe ya Kongo, MO Bejaia ya Algeria na Medeama wanajiandaa na mchezo wao wa tatu dhidi ya Medeama utakaochezwa July 15, kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Yanga muholanzi Hans van de Pluijm ameweka wazi mipango yake katika mazoezi

naifahamu Medeama vizuri sana na wana timu nzuri, wapo imara physical hivyo ukiniuliza vision zangu kama mwalimu hazitofautiani na makocha wengine, kama ilivyo kwa kocha yoyote ni kushinda mchezo na ndio ndoto na malengo yangu kwa sasa
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment