PICHA 3: Staa wa MAN United Kaanguka na Kupasuka Kwa Kula Chakula Cha Sumu

Beki wa kati wa klabu ya Manchester United ya England ambaye pia anachezea timu ya taifa ya England Chris Smalling jina lake limeingia kwenye headlines baada ya kuanguka na kupasuka sehemu ya juu ya jicho la kulia akiwa katika mapumziko yake Indonesia.  

Kwa mujibu wa mitandao mikubwa ya habari duniani kama dailymail.co.uk na mingine, imeripoti Smalling kuanguka na kupasuka sehemu ya jicho la kulia baada ya kula chakula ambacho kinatajwa kuwa kilikuwa na sumu.

Smalling alikuwa Bali na mpenzi wake Sam Cooke na alianguka na kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu, beki huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa kichwani kwake kawekwa bandeji kutokana na kuumia sehemu ya juu ya jicho la kulia.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment