Sakata
la Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL),
kugeuziwa kibao kwa kutakiwa kurejesha zaidi ya Dola za Marekani
milioni 100 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 216.2 kwa Shirika la Umeme
nchini (Tanesco), limezidi kuchukua sura mpya baada uongozi wa kampuni
hiyo kuibuka.
Kuibuka
kwa viongozi hao kumekuja siku chache baada ya Wakili wa Tanesco,
kueleza hatua watakazochukua kuhusu uamuzi huo baadaya Mahakama ya
Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID), uliotolewa Septemba 12
mwaka huu unaoitaka Tanesco kuilipa Standard Chartered ya Hong Kong
(SCB-HK) Dola za Marekani milioni 148.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti
ambaye pia ni Mwanasheria wa Kampuni wa IPTL, Joseph Makandege alisema
hawatambui madai ya Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK)
kama mdai na wala hawana haki kwa mujibu wa sheria.
Kutokana
na hali hiyo alisema inaungana na Shirika la Umeme nchini (Tanesco)
kukata rufaa katika Mahakama ya ICSID kwani hukumu iliyotolewa ina
mapungufu mengi ya kisheria.
Licha
ya uamuzi huo Makandege alisema IPTL haikulipwa kwa kutumia viwango vya
zamani bali walilipwa kutokana na umeme waliouuza kwa Tanesco na si
vinginevyo.
Alisema
watu wasifanye makosa kuilipa benki hiyo kwani inachotaka kufanya ni
kitendo cha utapeli kwa msukumo wa kampuni za mabeberu.
“Benki
ya Standard Chartered ya Hong Kong hawastahili kulipwa fedha na
Watanzania kwani hawastahili kwa mujibu wa sheria nasi kama IPTL/PAP
hatuwatambui na hawana haki ya kutuzungumzia. Na ndiyo maana wameamua
kukimbia mahakama zetu za ndani na kukimbilia nje, hawa wana msukumo wa
mabeberu wenye nia ovu.
“Kwa
uamuzi huu wenye utata uliotolewa na ICSID ni wazi Standard Chartered
walikuwa na nia ovu, ninasema hivyo kwa sababu tangu Septemba 5, mwaka
2013 suala hili liliamuriwa vizuri chini ya Jaji Utamwa (John) na IPTL
ikashinda kesi na kutwaa uongozi.
“Na
hili si la kwanza kwani Aprili 3, 2014 tulifungua shauri namba 60
chini ya Jaji Dk. Fauz Twalib la kuitaka Mahakama itamke kwamba benki
ya Standard Chartered Hong Kong si wadeni wetu, tena awali waliibuka na
hoja kwamba hawasikilizwi na Mahakama zetu za ndani kwa wakati ambapo
shauri hilo lilipangiwa kusikilizwa mfululizo.
“Lakini
pia dai letu lingine tuliomba Mahakama Kuu itupe nafuu ya Standard
kutulipa gharama kama fidia ya Dola za Marekani bilioni 3.240 ambapo
hata tuzo waliopewa na ICSID eti wanataka walipwe Dola za Marekani
milioni 148 na kama wakitulipa fedha zetu hata madai yao yaingia humo
nabado kuna fedha nyingine inabidi watupatiwe sisi,” alisema Makandege
Wakili
huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa niaba ya mmiliki wa IPTL/PAP,
Harbindar Singh Sethi mwenye makazi yake hapa nchini na Afrika Kusini,
alisema licha ya mahakama kutoa uamuzi wataendelea kusimamia uamuzi huo
wa kutomtambua mtu anayeitwa Martha Renju wala Benki ya Standard
Chartered ya Hong Kong.
“Sisi
msimamo wetu kama IPTL/PAP tunasema hadharani kwamba hatuitambua Benki
ya Standard Chartered ambao hawa kila wakati wamekuwa wakikimbia
mahakama zetu za ndani na kukimbilia nje na hata hukumu hii ya tuzo ina
viashiria vya mabeberu.
“Tuzo
husika waliyopewa ni dhahiri Standard Chartered ni batili kwa mujibu wa
sheria. Wao ni kina nani hadi wakafungie kesi kwa niaba yetu. Hii ni
kesi ya ngedere imepelekwa kwa nyani,” alisema
Kutolewa fedha za Escrow
Akizungumzia
mchakato wa kutolewa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, Makandege
alisema mchakato wa kutolewa kwa fedha hizo ulikuwa wa kihalali kwa
mujibu wa sheria za nchi.
Alisema
Julai 5, mwaka 2006, Serikali na IPTL waliingia mkataba wa Escrow ambao
ulipelekea kutolewa kwa fedha hizo kwenye akaunti hiyo iliyokuwa
imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) bila kuwahusisha Benki ya
Standard Chartered.
“Oktoba
8, 2010 IPTL na Tanesco kwa kuzingatia kipengele cha 10 cha mkataba huo
ambayo kinaeleza kuwa endapo kuna mgogoro baina ya pande hizo mbili
wahusika watakutana na kujadiliana na hatua ya kuafikiana itahesabika
kuisha kwa mgogoro.
“Hata
ripoti mbalimbali ikiwemo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) hakuna sehemu yoyote inayoeleza kuwa zile fedha ni za
umma. Hata ICSID imetoa hukumu na kusema si fedha za Serikali lakini
wanakiri zilitolewa kihalali ingawa hawakupewa Standard na kama
kungelikuwa na mgogoro fedha zile singetolewa,” alisema
Kunyang’anywa mitambo
Alipoulizwa
kuwa hatua ya suala hili kugubikwa na utata na utekelezaji wa maazimio
manane ya Bunge la 10 likiwemo la wao kunyang’anywa mtambo, Makandege
alisema wanajua kuna watu hivi sasa wanahaingika wakitaka kuona suala
hilo linafanyika.
Pamoja
na hali hiyo alisema kuwa mitambo bado ni mali yao kwa mujibu wa sheria
na hakuna hatua itakayowafanya wafanikiwe watu hao ambao hakuwataja.
“Tunajua
kuna watu hivi sasa wanataka kuona suala hili likitekelezwa ikiwemo
IPTL kunyang’anywa mtambo, ninawaambia hakuna jambo kama hilo, nasi kila
wakati tumekuwa wazi ikiwemo kulaani maazimio ya Bunge ambayo ni wazi
yalikuwa na lengo la kukimbiza wawekezaji wazawa. Suala hili hata Rais
mstaafu (Jakaya Kikwete) aliliweka wazi kwa nini lianze sasa baada ya
mjadala wake kufungwa,” alisema.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment