LOWASSA Azungumzia Utendaji Wa Rais MAGUFULI

Aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Edward Lowassa, amesema licha ya kukubali kazi za Rais John Magufuli, yapo maeneo ambayo yana mapungufu.
Ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na ripota wa BBC mjini Nairobi na aliweza kujibu maswali kadhaa. Moja ya maswali hayo ni pamoja na anavyouchukulia utendaji wa Dkt Magufuli.
“Kuna maeneo anafanya vizuri, kuna maeneo ambayo naamini tungefanya vizuri zaidi, hili niishie hapo, anafanya vizuri kiasi gani ameshindwa kiasi gani tuwaachie wataalamu wengine wachambue”, alisema Lowassa.

Watu tofauti tofauti wamekuwa wakitoa maoni juu ya utendaji kazi wa Rais Magufuli huku wakiendelea kufurahishwa na utendaji kazi wake, kama kutetea wanyonge, kuanzisha ya elimu bure na mengine. Kwa mujibu wa utafiti mpya wa Twaweza, asilimia 96 ya Watanzania wanapendezwa na utendaji wake.
BY: EMMY MWAIPOPO
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment