Mawaziri Wa John MAGUFULI Waonywa!

DODOMA: Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ana orodha ya wabunge na mawaziri waliokithiri kwa utoro bungeni, hivyo kuwataka kubadilika huku akitishia kuwaanika na kuwashitaki hadi kwa Rais John Magufuli.

Alisisitiza kutotania katika suala hilo na kuongeza kuwa mahudhurio katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 unaotarajiwa kuanza Novemba mosi mwaka huu, ndiyo utakaokuwa kipimo chao cha mwisho.

Aliyasema hayo bungeni jana muda mfupi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuahirisha vikao vya Mkutano wa Nne wa Bunge hilo lililokutana kwa wiki mbili kuanzia Septemba 6, mwaka huu.

“Kuna orodha nimeiandaa ya watoro katika kamati, lakini kwa leo sitawataja hapa kwa sababu nimeona tuendelee kuwafuatilia katika vikao vijavyo. Kama hawatabadilika nitawaambia waajiri wao, yaani wabunge watoro nitawasema kwa wananchi wao na kwa viongozi wa vyama vyao na kwa mawaziri watoro, nitamwambia namba moja, kwamba mawaziri hawa hawawajibiki ipasavyo.” Alisisitiza.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment