Utafiti huo uliopewa jina ‘Rais wa Watu’ ulijikita katika tathmini na matarajio kwa wananchi kwa rais huyo wa awamu ya tano.
“Watu wanakubali hatua zinazochukuliwa na uongozi wa awamu ya tano wa rais John Pombe Magufuli, hususan katika kuondoa wafanyakazi hewa, sera ya elimu bure, na uhamasishaji wa wafanyakazi wa watumishi wa serikali kutokana na makosa mbalimbali,” alisema Mkurugenzi wa Twaweza, Aidan Eyakuse.
Miongoni mwa vitu alivyoahidi Rais Magufuli ni wanafunzi kusoma bure akiwa mastari wa mbele kupinga vitendo vya rushwa.
BY: EMMY MWAIPOPO
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment