Watu wawili wamekufa katika matukio mawili tofauti, akiwamo mtoto Mariam
Haule (2) kwa kunyongwa na baba yake wa kambo baada ya kumtuma mama
yake dukani kisha kutokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea Mei 2.
Issa
alisema kuwa mtuhumiwa huyo mkazi wa Kijiji cha Usimba, Wilaya ya
Kaliua mkoani humo kabla ya kufanya mauaji hayo, alimtuma mkewe, Kalunde
Malugu kwenda dukani kununua dawa .
Alisema baada ya mkewe kwenda dukani, alipata mwanya wa kufanya mauaji hayo kisha kutokomea kusikojulikana.
“Tunawaomba
wananchi waendelee kutoa ushirikiano ili tuweze kumkamata mtuhumiwa
afikishwe kwenye mkondo wa sheria,” alisema Issa.
Kamanda huyo alisema jeshi hilo litahakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.
Mama
wa mtoto huyo alisema alitumwa na mumewe dukani kununua dawa, lakini
aliporudi alikuta mlango umefungwa na alipoingia ndani alibaini mtoto
wake ameuawa.
Alisema hafahamu sababu za mauaji hayo na wala
hakukuwa na malalamiko au madai yoyote kutoka kwa mumewe kuhusiana na
mtoto huyo.
Katika tukio la pili; Mkazi wa Kijiji cha Rwamkoma
wilayani Butiama, Magesa Machera (46) amekutwa ameuawa kwa kunyongwa
baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema tukio hilo lilitokea Mei 3, mwaka huu saa tisa usiku.
Alisema
inadaiwa kuwa siku ya tukio hilo, mpenzi wake, Remmy Samwel (35)
alitoka nje kwenda kujisaidia, lakini aliporudi alimkuta Machera akiwa
chini amekufa.
Ng’anzi
alisema mpenzi wake huyo ambaye ni mgeni katika kijiji hicho huwa na
mazoea ya kwenda kumsalimia mara kwa mara na walikuwa wakinywa pombe za
kienyeji. “Uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea na polisi inamshikilia
mpenzi wake,” alisema.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment