Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyokuwa ikipinga kuondolewa kwa shitaka
la 8 la utakatishaji fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake wawili.
Uamuzi
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Jaji Mfawidhi wa Mahakama
hiyo, Mheshimiwa Moses Mzuna alipokuwa akitoa majibu ya rufaa iliyokuwa
imekatwa na DPP.
“Ninafahamu
kila kesi inaamuliwa kutokana na mazingira yake lakini nimefuta rufaa
hii kwa kuwa hoja zilizotolewa hazina nguvu kisheria” alisema Jaji Mzuna.
Aidha
Jaji Mzuna amefafanua kuwa hata kama amefuta rufaa hiyo lakini upande
wa Jamuhuri bado una nafasi ya kubadilisha shitaka au hati nzima ya
mashtaka inayowakabili washtakiwa hao.
Kwa
upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Timony Vitalis amekubaliana na
uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu ya pingamizi lake ingawa bado
anasimamia watuhumiwa kutofutiwa shitaka la utakatishaji wa fedha.
Naye
Wakili wa Utetezi Majula Magafu amesema kuwa wao wanasubiri maamuzi
yatakayotolewa na Wakili wa Serikali ili wajue namna ya kuikabili kesi
hiyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment