Na Raymond Mushumbusi -MAELEZO
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imewakamata zaidi wafanyabiashara 300 kwa kosa
la kutotumia mashine za (Electronic Fiscal Devices) EFD’S katika
biashara zao.
Akizungumzia
na waandishi wa habari Jijini Dare s Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema mamlaka yake imefanya
uchunguzi wa kina na kuwabaini wafanyabiashara hao katika maeneo
mbalimbali nchini wakikiuka agizo la kuwa na mashine hizo.
“Tumeshaanza
kuwapeleka mahakamani wafanyabiashara ambao wanakwepa kulipa kodi kwa
kuuza bidhaa bila risiti na pia tumetaifisha bidhaa mbalimbali
zilizoingizwa nchini kwa njia ya magendo na kukwepa kodi “ Alisema Kidata.
Kamishna
Kidata amefafanua kuwa mamlaka haitowavumilia wafanyabiashara
wanaoikosesha mapato Serikali kwa kuuza na kutoa huduma bila risiti za
EFD’s kwa makusudi na hasa wale wafanyabiashara wanaouza kazi za wasanii
bila stempu za kodi pamoja na wafanyabiashara wanaojihusisha na
magendo.
Vilevile
amefafanua kuwa, kwa wafanyabiashara waliopelekwa mahakamani mara baada
ya kumalizika kwa kesi zao na kupewa adhabu ya kulipa faini,
wakibainika tena kurudia makosa hayo adhabu kali zaidi zitachukuliwa
dhidi yao ikiwemo kifungo cha miaka mitatu jela kwa kukaidi agizo la
Serikali.
Aidha,
Mamlaka imetoza faini ya Shillingi Mil 746 kwa wafanyabiashara
waliokutwa na makosa mbalimbali yakiwemo kutotumia mashine za
kielotroniki za EFD’s , kuingiza bidhaa kimagendo na kuuza kazi za
wasanii bila ya stempu ya kodi.
Mamlaka
inatoa wito kwa wananchi wote kuwa mabalozi wa kodi na kichocheo cha
ukusanyaji wa mapato kwakutimiza wajibu wao wa kudai risiti wanaponunua
bidhaa au kupatiwa huduma mbalimbali.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment