Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Sergio Aguero amesema kuwa
atahama klabu hiyo wakati mkataba wake utakapokamilika Raiya huyo wa
Argentina ana mkataba wa miaka mitano ambao utamalizika katika msimu wa
2018-19.

Amesha ifungia City mabao 128 tangu aliposajiliwa na klabu hiyo
kutoka Atletico Madrid kwa kitita cha pauni milioni 38 mwaka 2011,na
kushinda ubingwa wa ligi ya Uingereza mara mbili.
Aguero mwenye miaka 27 alikiambia kituo kimoja cha redio nchini
Argentina kwamba ni wazi atarudi katika kilabu yake ya kwanza ya
Independente na kustaafu.
”Hapa City wanajua ni nini ninacho taka kufanya,wanajua nataka kurudi Argentina”,aliongezea.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment