
Polisi
Kanda maalum Dar es salaam kupitia kitengo cha usalama barabarani
wametoa taarifa ya makosa ya barabarani kuanzia March 07 2016 hadi March
18 2016 kuwa wamefanikiwa kukamata magari mbalimbali kwa makosa ya
usalama barabarani na jumla ya Tsh Milioni 577.8 zimekusanywa ikiwa ni
tozo kwa makosa hayo kwa muda wa siku 11.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema…..>>>‘madereva
wametakiwa kuwa waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu
zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku’
Aidha hapo awali Kamishna Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro alitoa
taarifa ya kukamata madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa
kilo moja katika eneo la Mbezi beach ambapo Jeshi la polisi
linamshikilia pia mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la Benson Muro Charles, mwenye umri wa miaka 32.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment