Habari za kutekwa kwa mwandishi wa habari wa idhaa ya kiswahili ya DW ya Ujerumani Salma Said visiwani Zanzibar
zilizidi kuenea katika kila kona huku kila mmoja akiwa hajui alipo
mwandishi huyo, ila March 21 kumetoka habari njema za kupatikana kwa
mwanadishi huyo.
Salma Said amepatikana na kuongea kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari baada ya kutekwa kwa zaidi ya siku mbili “Nitaeleza
kwa kifupi sana kwa sababu ni uhuni na unyama niliyofanyiwa, nilitekwa
wakati nipo Airport nikisubiri gari yangu ije kunichukua, ndipo
waliponichukua kwa nguvu na kupandishwa katika gari yao” >>> Salma Said
“Jana
ndio wakanirudisha nilipokuwa karibu na kituo cha Tax cha Airport
ilikuwa saa 11 alfajiri huku usoni nikiwa bado nimefunikwa, nikajiburura
hadi barabarani na kumuomba msaada mama mmoja ambae aliniambia kaa
chini mwanangu” >>> Salma Said
Video ya Salma Said akieleza namna ilivyokuwa
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment