Prof. Beno Ndulu: Watu Wanaongea Wasiyoyajua, BOT Haina Wafanyakazi Hewa!

Hatimaye gavana wa BOT Prof. Beno Ndulu ametoa majibu kwa rais John Magufuli huku akisisitiza kuwa watu wanaongea wasiyoyajua na kuomba apewe majina pamoja na taarifa za wale watu wanaodhani kuwa ni wafanyakazi wasio na umuhimu BoT.

Hayo yanajiri siku moja baada ya rais John Magufuli kumuagiza gavana huyo kuwaondoa ndani ya utumishi wa BoT wafanyakazi wote wasio na umuhimu pamoja na wale wanaojulikana kuwa ni wafanyakazi hewa.

Jana gavana akiongea na vyombo vya habari pamoja na gazeti la MTANZANIA alisema kuwa kila mfanyakazi wa BoT ana umuhimu wake huku akisisitiza kuwa watu wanaongea wasiyoyajua. Prof. Ndulu pia alisisitiza kuwa yule anayedhani kuwa kuna wafanyakazi wasio na umuhimu BoT basi ampelekee majina yao pamoja na taarifa zao!

Hata hivyo gavana huyo aliweka wazi kuwa rais ametoa agizo hivyo ni muhimu kuzingatia agizo la rais lakini akaweka mkazo kuwa BoT itajiridhisha kwa kina kwanza kabla ya kuchukua hatua yoyote ile!
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment