Moja kati ya watu walio wekewa X hizo kwenye nyumba yake amesema wamelala walipo amka walijikuta nyumba zao zikiwa tayari zina X na kuekewa kipeperushi hicho cha onyo.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Kusini Pemba ilifika kijijini Pujini Kumvini na Kijili kujionea nyumba hizo zilizo wekewa X nyekundu ampapo mwenyekiti wakamati hiyo mkuu wa mkoa Kusini Pemba Bio Mwanajuma Majidi Abdalla amewataka watu wanao taka kwenda kupiga kura waende kupiga kura na kuzipuzia X hizo huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.
Bimwana Juma amewataka wanaume wasiwatishe wana wake kwa kutishia talaka kwa sababu ya kwenda kupiga kura badala yake wawape uhuru wanawake kuamua pindi wakitaka kwenda kwenye uchaguzi waende pasi vitisho vya vua aina yoyote.
Nae kamanda wa polisi mkoa kusini pemba kamishimna msaidi mohamed shekhan mohamed amesema jeshi lake halitishiki na vitendo vya aina hio na kwamba watawakamata wale wote waliohisika na uwekaji wa x hizo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment