Akizundua taarifa ya utafiti huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema utafiti huo umelenga kupata takwimu sahihi za idadi ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi na wale ambao hawewezi kufanya kazi za uzalishaji zenye kuleta tija kwa wao binafsi na taifa kwa ujumla.
Mhe. Jenista Mhagama amesisitiza kuwa takwimu zilizopatika katika utafiti huo zinaonesha ni namna gani watanzania wanashindwa kujishughulisha katika kufanya kazi zenye kuwaingizia kipato na badala yake wanatumia muda wao mwingi kufanya shughuli zisizo za uzalishaji hasa kufanya starehe mbalimbali.
“Ndugu zangu watanzania unakuta mtu amekaa baa au anacheza poll table kuanzia asubuhi mpaka jioni na hujui anafanya kazi gani ya uzalishaji, ndugu zangu tuone aibu basi tujishugulishe tulijenge taifa letu ili kujiletea maendeleo yetu na nchi yetu.”
Aidha matokeo ya utafiti huo yanaeleza kuwa asilimia 18.5 ya wananchi ambao wanafanya kazi za uzalishaji na asilimia 10.6 ni wale wanaofanya shughuli za nyumbani zisizo na malipo, na uchambuzi wa kijinsia unaonesha kuwa wanaume asilimia 23.8 wanatumia muda wao mwingi zaidi kwenye shughuli za kiuchumi ukilinganisha na asilimia 13.5 ya wanawake na kwa upande mwingine wanawake asilimia 16.5 wanatumia muda wao mwingi kufanya kazi za nyumbani zisizo na malipo ukilinganuisha na asilimia 4.4 ya wanaume.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment