Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema
Serikali haitaongeza muda katika zoezi zima la uzimaji wa simu feki
ifikapo Juni 16 mwaka huu.
Ameyasema hayo ofisini kwake leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha habari hapa nchini.
Amesema
Serikali imeamua kuchukua uamuzi huo kutokana na madhara mbalimbali
yatokanayo na simu hizo ikiwemo ya kiafya na kusisitiza kuwa serikali
inapoteza mapato mengi kutokana na uingizwaji wa simu hizo nchini.
"Tunategemea
kuzima simu zote feki kutokana na madhara yake kiafya hasa kwa
watumiaji, kukosekana kwa viwango vya ubora wa simu hizi na hivyo
wananchi kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa simu hizi kwani
hufa mara kwa mara", amesema Waziri Mbarawa.
Aidha,
Profesa Mbarawa ameongeza kuwa kwa sasa Jopo la wataalamu kutoka
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) limepelekwa mkoani Singida kwa
ajili ya kutoa elimu ya utambuzi wa simu hizo ili kuweza kuwasaidia
wananchi kubaini kwa urahisi.
Amesisitiza
wananchi kuchukua tahadhari kabla ya kununua simu ikiwemo kumuuliza
muuzaji kabla ya kununua, kudai risiti na kuituinza ili kudhibiti
uingizwaji na usambazaji wa bidhaa hizo nchini.
Katika
hatua nyengine, Waziri Mbarawa amesema kuwa suala la mkongo wa Taifa
linaendelea vizuri ambapo Serikali kwa kushirikiana na watoa huduma wa
mawasiliano wanaendelea na usimikaji wa minara ya mawasiliano katika
sehemu mbalimbali za nchi hususan vijijini ili kuleta huduma bora za
mawasiliano nchini.
"Kwa
sasa awamu ya nne ya mradi huu wa Mkongo wa Taifa unaendelea, kwani
makampuni mbalimbali ya simu yanasimika minara yao katika sehemu
mbalimbali za nchi ili kusambaza na kuboresha mawasiliano kwa wananchi", amefafanua Profesa Mbarawa.
Ameongeza
kuwa uwepo wa mkongo huo nchini kumepelekea mapinduzi katika sekta ya
mawasiliano, mabenki na kuiongezea Serikali pato kwani hata nchi za
jirani hutumia mkongo huo katika kupata mawasiliano yaliyo bora.
Tathmini
imebainisha kuwa kutokana na uwepo wa mkongo huo nchini watumiaji wa
simu wamefikia milioni 39.7 na wa intaneti kufukia milioni 17.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment