Didier DROGBA Kuishtaki Daily Mail

Drogba Foundation (3)
Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Daily Mail.
Hii ni baada ya gazeti hilo kuchapisha habari zinazodai kwamba kati ya pesa anazokusanya kupitia wakfu wake wa kusaidia jamii, ni chini ya asilimia moja zinazotumiwa kufaa jamii.
Drogba Foundation (5)
Gazeti hilo limesema ni £14,115 pekee kati ya £1.7m zinazotolewa na wachezaji nyota na wafanyabiashara ambazo husaidia watoto Afrika.
Drogba Foundation (4)
Drogba, 38, ametoa taarifa akisema habari hizo ni za “uongo na za kumharibia sifa”.
Tume inayodhibiti mashirika ya kusaidia jamii yaliyosajiliwa Uingereza imesema inachunguza “madai ya ukiukaji wa sheria”.
Drogba Foundation (2)
Kwenye taarifa yake, Drogba amesema: “Hakuna ulaghai, hakuna ufisadi na hakuna udanganyifu.”
Drogba Foundation (1)
Drogba, raia wa Ivory Coast, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Canada kwa sasa amewatuhumu wanahabari wa Daily Mail kwa kuweka hatarini maisha ya maelfu ya watoto wa Afrika.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment