Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando (kushoto)
akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Jana
, ambapo alisomewa shitaka la matumizi mabaya ya madaraka. (Picha na
Maktaba)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia
huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),
William Mhando, mkewe Eva Mhando na mtoto. Mhando na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa makosa sita likiwemo la matumizi mabaya ya ofisi, hivyo kulingana na ushahidi walioutoa mahakamani, umeonyesha dhahiri kwamba hawana hatia na wameachiwa huru.
Kesi yao imesomwa na Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi hiyo Kwei Lusema.
Wakati huo huo, Wakili wa Serikali aliyekuwa anasimamia kesi hiyo, Leonard Swai kwa njia ya simu amesema rushwa iliyopo mahakamani inatisha na serikali inatakiwa kuchukua hatua.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment