RAIS WA ZFA KUJULIKANA LEO

UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Taifa unatarajiwa kufanyika leo.
Uchaguzi huo utakaohusisha nafasi za Rais na Makamu wawili, mmoja kutoka Unguja na mwingine wa upande wa Pemba, utafanyika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo kilichopo Wawi, Kisiwani Pemba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Suleiman Haji Hassan alisema kwa upande wao kamati wameshamaliza taratibu zote na wanachosubiri ni kusimamia uchaguzi tu.
Alisema kuwa tayari wajumbe wote wa kamati ya Uchaguzi wameshawasili Pemba na maandalizi kwa upande wao yapo vizuri.

Aliongeza kuwa, waliomba kuwania urais ni Salum Bausi na Rais aliyemaliza muda wake, Ravia Idarous Faina, wakati wanaowania Umakamu wa Rais wa ZFA kwa upande wa Pemba ni Ali Mohammed na Suweid Hama, wakati kwa upande wa Unguja ni Mzee Zam Ali, Mohammed Masoud na Ali Salum Nassor Mkweche.
Viongozi ambao watateuliwa katika uchaguzi huo wanatarajia kukitumikia chama hicho kwa kipindi cha miaka minne ijayo ya uongozi wao kwa mujibu wa katiba.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment