Baada ya TFDA Kufungia Machinjio Vingunguti, Mawaziri Wamefika na Kutoa Maamuzi Haya

April 17 2016 Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba aliongozana na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mpaka kwenye machinjio ya Vingunguti Dar baada ya machinjio hayo kufungiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kwa kutozingatia usalama na usafi wa maeneo ya machinjio.

Baada ya kikao cha muda mfupi kilichofanyika kwenye machinjio ya Vingunguti Waziri Nchemba aliyaongea haya ‘Kwanza kuna mambo kadhaa tumeyaona ambayo TFDA wamefanya kazi nzuri sana nawapongeza sana wamebaini ukosefu wa maji, na pia visu vinavyotumika kuchinjia vinasafishwa mahali ambapo sio salama vinasafishwa bafuni‘ >>>Mwigulu Nchemba Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji

”Kwa hiyo nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa nyama itakayokuwa kwenye mabucha itakuwa ni nyama salama lakini tutahakikisha tunaendelea kulinda viwango vya nyama ili wasiweze kupata madhara ya kiafya‘>>>Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment