Kwa Mujibu wa Mbunge Mtulia aliwaambia Wananchi wake kuwa mpaka sasa Mwanasheria Abubakari Salum anaye isimamia kesi hiyo ameshamaliza taratibu za kuishtaki Serikali baada ya kuonekana Agizo la Kuvunjwa Nyumba lilifanywa kimakosa na hivyo muda wowote kuanzia sasa kesi itarindima mahakamani kinachosubiriwa ni kupangiwa tarehe ya kesi.
Hata hivyo Mbunge Huyo alisema katika kesi hiyo wataishawishi Mahakama waathirika wa zoezi hilo Seriali inawalipa fidia, lakini mbali na hayo mpaka sasa waathirika wote waliobomolewa nakutelekezwa kwenye vibanda, wameandaliwa mpango maalumu ili kunusuru Maisha yao.
Mbali na suala la Bomoa bomoa, Mbumge alitumia muda mwingi kuwasisitiza kuijunga na Bima ya Afya ambayo kwasasa inapatikana Jimboni kwake kwa Ada ya gharama ya shilingi elfu 40,000 kwa mzima.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment