Hawa Hapa Viongozi wa Juu wa TFF Waliokuwa Wakiomba Mil 25 ili Kupanga Matokeo.. [+Audio]

Mambo mapya yamezidi kuibuka kuhusu sakata la upangaji matokeo kwenye ligi daraja la kwanza ikiwa ni siku chache baada ya TFF kutoa hukumu kwa baadhi ya viongozi, wachezaji na waamuzi waliopatikana na hatia mbele ya kamati ya nidhamu ya Shirikisho hilo linalosimamia mpira wa miguu Tanzania.

Kubwa ambalo ndiyo habari ya ‘mujini’ kwa sasa ni kuvuja kwa sauti ambayo wanasikika baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa TFF pamoja na viongozi wa timu ya Geita Gold Sports wakipanga mikakati ya kupanga matokeo ambayo inahusisha rushwa ndani yake.

Sauti ya kigogo mmoja wa TFF inasikika akiomba rushwa ya shilingi milioni 25 kutoka kwa viongozi wa Geita ili aweze kuhakikisha anawasaidia katika baadhi ya matatizo ambayo miongoni mwayo ni pamoja na vibali vya wachezaji.

Sauti hiyo imeifikia www.shaffihdauda.co.tz na kutokana na kutaka kuwajulisha wadau wa mchezo huu pendwa, mtandao huu unakuletea moja kwa moja sauti hiyo ili upate kuwasikia vigogo hao wa TFF wenye dhamana kubwa ya soka la Bongo wanavyolihujumu na kulisambaratisha soka kwa kutumia vibaya mamlaka yao.

Jana (April 5) Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha alitangaza kujiuzulu nafasi yake katika utumishi wa TFF mara baada ya kuvuja kwa sauti ya mjadala wa kupanga matokeo pamoja na kuomba rushwa.

Katika barua yake aliyomwandikia Katibu Mkuu wa TFF, Chacha alieleza kuwa amepata majukumu mapya ya kikazi ambayo pamoja na majukumu ya kifamilia yatamfanya akose muda wa kutumika vema katika nafasi yake katika Shirikisho.

Martin alijiunga na TFF Julai 2014 akiwa Afisa wa Mashindano na baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano, kufuatia aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo Boniface Wambura kuteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Hili ndiyo soka la Bongo sinema na mazingaombwe bado yanaendelea TFF, usiache kufatilia www.shaffihdauda.co.tz kujua mengi zaidi juu ya sakata hili, utaendelea kupata taarifa kadiri zinavyotufikia kutoka katika vyanzo mbalimbali.
Hii hapa ndiyo sauti iliyonaswa kwenye mjadala huo wa upangaji matokeo uliowahusisha maafisa wa ngazi za juu wa TFF pamoja na viongozi wa timu ya Geita Gold Sports ya mkoani Geita.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment