Hili Ndio Gazeti Lililothibitisha JOSE MOURINHO Kusaini Mkataba na MAN United


Kwa sasa ukisikia jina la kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho kitakachokujia kwa haraka haraka ni timu gani atajiunga nayo baada ya kufukuzwa kazi na Chelsea, mengi yameandikwa kuhusu Jose Mourinho kuwa katika mpango wa kujiunga na Man United mwisho wa msimu.

Bado uongozi wa Man United na Mourinho hawajazungumza chochote juu ya tetesi hizo zaidi ya Jose Mourinho kuthibitisha tu atarudi kazini mwisho wa msimu bila kutaja atakuwa na klabu gani. April 23 2016 habari kutoka gazeti la Ureno Jornal de Noticias ni kuwa Jose Mourinho amesaini Man United.
Gazeti hilo linatajwa kuandikwa kwa kireno na kutafrisika hivi ‘Jose Mourinho amesaini Man United’ stori zinaeleza zaidi kuwa Jose Mourinho ameshaanza kusaka wachezaji kwao Ureno kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi cha Man United akisaIdiwa na msaidizi wake Rui Faria.

Stori hizi bado zinatajwa kama tetesi lakini ukweli au uzito wa habari kutoka gazeti hili unapata nguvu kutokana na Jose Mourinho kwao ni Ureno, hivyo huenda ikawa stori zimevuja, sio Jose Mourinho wala mtendaji mkuu wa wa Man United Ed Woodward waliokubali kuzungumzia chochote kuhusu taarifa, yaani hata kukanusha.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment