Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George
Simbachawene amesema mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), unatarajia
kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu.
Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara
ya Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Simbachawene
alisema baada ya kukutana na wadau wa mradi huo, wamewahakikishia kuwa
utaanza rasmi mwezi ujao bila kukosa.
“Tumeambiwa mradi huu una mikataba
mingi na kuwa bado kuna mjadala mkubwa wa mikataba. Hatuwezi kulazimisha
maana unaweza kujikuta ukitengeneza mikataba mibaya, hivyo tunaendelea
na mijadala ya mikataba,” alisema.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson
Rweikiza alisema wameutembelea mradi huo zaidi ya mara nne na kugundua
tatizo linaloukwamisha kuwa ni fedha na kuitaka Serikali kutoa fedha ili
uanze.
Aliesema lengo la kuanzishwa kwa mradi
huo ni kupunguza kero ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
wanaokabiliwa na tatizo la usafiri na foleni za barabarani, hivyo
kutumia muda mrefu barabarani.
Rweikiza alisema kukamilika kwa mradi
huo na kuanza kufanya kazi kutapunguza kero na kuokoa muda mwingi
uliokuwa ukitumia bila uzalishaji.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment