Roboti wa kike (kulia mwenye nguo nyekundu) aliyetengenezwa na Chen Xiaoping na kumpa jina la Jia Jia lenye maana ya mungu.
Wanahabari wakiongea na roboti huyo.
Wanahabari wakimpiga picha.
UNAWEZA
kushangaa lakini ndiyo ukweli wenyewe kwamba jamaa mmoja anayejulikana
kwa jina la Chen Xiaoping amefanikiwa kutengeneza roboti wa kike na
kumpa jina la Jia Jia lenye maana ya mungu roboti wa kike.
Chen Xiaoping anasema kwamba kwa kipindi kirefu amekuwa akiwaona watu
wakitengeneza maroboti wenye vyuma hivyo alichokuwa akifikiria ni
kutengeneza roboti na kisha kumvisha ngozi, aonekane kama binadamu, na
kweli akafanikiwa kwa asilimia kubwa.
Ukimwangalia roboti huyu, ni vigumu kumgundua kwani ana kila kitu kwa
nje ambacho binadamu wa kawaida anacho. Lengo lake la kutengeneza
roboti huyo hakusema, kama ni kufanya kazi au vitu vingine ila kitendo
cha kutengeneza roboti huyo kimempa heshima kubwa kijana huyo aliyekuwa
akisoma katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia hapohapo China.
Source: Daily Mail, England.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment