Sadiki
alifika wilayani Hai jana, ikiwa ni moja ya ziara zake katika wilaya
zote za Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na
kuzungumza na viongozi mbalimbali wanaowakilisha wananchi, pamoja na
kusikiliza kero zinazozikabili wilaya hizo.
Katika
kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri, Usharika wa Hai Mjini, madiwani hao ambao wote ni wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hawakuonekana hata mmoja huku eneo
walilokuwa wameandaliwa likibaki na viti vilivyo wazi.
Awali,
Mkuu wa Mkoa alipowasili ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa lengo la
kupokea taarifa ya wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mchomvu aliwasili
kwa kuchelewa na muda ulipofika wa kuelekea ukumbini, alitokomea
kusikojulikana.
Hali
hiyo ilimshangaza Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ambaye
alisema siasa ziliisha baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana,
lakini inashangaza kwenye masuala ya maendeleo ya wananchi bado viongozi
wanaendelea kuziendekeza.
Byakanwa
alisema, licha ya madiwani wote 17 wanaounda Baraza la Madiwani Wilaya
ya Hai kuwa ni wa Chadema, bado wanasimamia na kutekeleza Ilani ya Chama
Cha Mapinduzi ambacho ndicho chama kilichopewa ridhaa na Watanzania
kuongoza kwa awamu nyingine ya tano.
“Ni
jambo la kushangaza kuona viongozi waliochaguliwa na wananchi
wanashindwa kuwakilisha wananchi wao katika kupeleka na kuzisemea kero
zao mbalimbali zinazowakabili, na badala yake wamekuwa wakisusa vikao
vya kupanga maendeleo. Kwa siasa hizi wananchi hawawezi kupata
maendeleo,” alisema Byakanwa.
Akiwasilisha
taarifa za kutofika kwa madiwani hao, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Hai,
Rosemary Kuringe alisema, amewasiliana na madiwani wake na kuelezwa
kuwa hawakupata taarifa za ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa.
Akijibu
baadhi ya maswali yaliyoulizwa na viongozi mbalimbali, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Saidi Mderu alikiri kutoa
taarifa kwa madiwani wote katika kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani
kilichofanyika Aprili 22, mwaka huu.
“Kwa
suala hili la viongozi hawa kususa, namwachia Mungu, niliwapa taarifa
madiwani wote tena nilisisitiza, cha kushangaza wakati Mkuu wa Mkoa
amewasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri
alifika akiwa amechelewa lakini wakati tumekuja kwenye ukumbi
hatukumuona,” alisema Mderu.
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Hai,Said Mderu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment