Polisi Kutumia FastaFasta Kudhibiti Matukio ya Kihalifu Nchini Tanzania

Huduma ya kwanza kuanzishwa nchini, FastaFasta Application inayopatikana katika simu za mkononi ‘Smart phone ‘ imetajwa kuwa suluhisho la usalama barabarani pamoja na kupunguza vitendo vya uhalifu kwa abiria na madereva wa vyombo vya usafiri vinavyosajiriwa katika huduma hiyo.

Huduma ya FastaFasta APP hadi sasa imesajiri zaidi ya tax 250, bajaji 150, na Bodaboda 100 ambazo kwa sasa zinatoa huduma katika jiji la Dar es Salaam, na kwamba inatarajiwa kutolewa katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Moshi, Mbeya na Tanga siku za hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Kikosi cha Usalama Barabarani SACP Fortunatus Musilimu alisema kuwa huduma hiyo itawarahisishia kupata idadi ya vyombo vya usafiri pamoja na kubaini wahalifu wanaotumia vyombo hivyo hasa bodaboda pindi watakapofanya matukio ya uhalifu.

“Huduma hii inamrahisishia mteja kumjua vizuri dereva atakayemhudumia na kwamba endapo atasahau mzigo au kufanyiwa uhalifu wowote ni rahisi kuchukua hatua kwa sababu taarifa zake zitakuwa rahisi kupatikana,” alisema.

Alisema pia madereva wanaojisajili katika huduma hiyo wanapatiwa elimu ya usalama barabarani na kwamba elimu hiyo itawasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Mtendaji upande wa teknolojia katika huduma ya fastafasta, Pius Paul madereva watakaojiunga katika huduma hiyo watarahisishiwa upatikanaji wa abiria wa uhakika huku akiwataka wananchi kuipakua huduma hiyo kwenye simu zao za mikononi hasa smart phone ili wasipate usumbufu pindi wanapphitaji usafiri wa haraka.

“Gharama yake ni nafuu kwa pande zote mbili, mteja na dereva, dereva atakayejisajili kwenye huduma hii atatozwa asilimia 15 ya bei anayomtoza mteja na kwamba asilimia 85 inayobaki ni ya kwake,” alisema Pius.

Alsaba Rahman, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara ‘PAMOJA APP’ alisema wameandaa tamasha linalofahamika kwa jina la Pamoja Festival kwa kushirikiana na huduma ya FastaFasta linayotarajiwa kufanyika Septemba 24, 2016 ambalo linalenga kukusanya wadau wa usafirishaji pamoja na wananchi litatoa elimu ya masuala ya usalama barabarani.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment