Tanzania imewapokea wafanyabiashara 50 kutoka Urusi kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali nchini.
Akieleza
ujio wa wafanyabiashara hao, Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji wa
Wizara ya Viwanda na Biashara, Adolf Mkenda alisema baada ya
kushirikiana kisiasa kwa muda mrefu, Urusi imeamua kuisaidia Tanzania
kuimarisha uchumi wake.
Wafanyabiashara hao wanatarajia kukutana
leo katika kongamano litakalobainisha fursa zilizopo kwa wageni hao
kuwekeza hasa kwenye kilimo, nishati, usafiri, viwanda na madini.
Urusi
ni miongoni mwa mataifa 10 makubwa kiuchumi duniani na imeendelea
kisayansi na kiteknolojia huku ikiwa na idadi kubwa ya watu.
Rais
mstaafu, Jakaya Kikwete wakati akiwaaga mabalozi 36 wa Tanzania,
aliwaagiza kulitangaza Taifa huko waliko ili kuvutia wawekezaji na
kuwaongezea masoko Watanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Urusi,
Wynjones Kisamba ameanza kuonyesha njia kwa ugeni huo unaotarajia
kuongeza biashara za Taifa hilo.
Mkurugenzi wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC), Julieth Kairuki alisema Watanzania wana uhakika
na soko la mbogamboga, matunda, asali na bidhaa nyingine nchini humo na
kwamba kinachotakiwa ni kuongeza ubora ili kukidhi viwango vya
kimataifa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment