Mambo 8 Muhimu Kuhusu Huduma Mpya ya WhatsApp

KUTOKANA na tatizo la kuingiliwa kwa mawasiliano ya watumiaji wa WhatsApp, hivi karibuni kampuni hiyo ilianzisha huduma ya end-to-end encryption ili kuboresha huduma zao za mawasiliano hasa katika nyanja ya kuimarisha ulinzi wa mawasiliano ya wateja wao.
1. End-to-end encryption ni nini?
Hii ni huduma mpya ya WhatsApp inayotumiwa kwa ajili ya kulinda mawasiliano baina ya mtumaji na mpokeaji kwenye mtandao huo bila mtu wa kati kuingilia mawasiliano hayo. huduma hii pia inapatikana iwapo mtumianji wa ataingiza toleo jipya la WhatsApp. Inatumika kwenye simu zote za iOS na Android.
2. Unawezaje kuwezesha (activate ) huduma hii?
Haya yote yanafanyika kwa mfumo kujiendesha wenyewe (automatically), hauhitaji kufanya mpangilio (setting) ili kuwezesha usiri wa mawasiliano yako.
3. Je, huduma hii pia inahusisha upigaji simu wa kwenye WhatsApp call?
Ndiyo, kama meseji zako zinalindwa hata WhatsApp calls pia zinalindwa kwa mfumo wa end-to-end encryption ambapo mpigaji wa simu na mpokeaji ndiyo wataweza kuwasiliana wakati mtu wa kati (third part) hatakuwa na uwezo wa kuona wala kusikia mawasiliano hyo.
4. Vipi kuhusu midia?
Media zote ambazo ni video, audio, picha na mafaili pia yatakuwa na ulinzi kutoka kwa mtumaji kwenda kwa mpokeaji.
5. Vipi kuhusu Magrupu?
Group halitawekewa ulinzi mpaka ambapo mmoja kati ya members atakapokuwa na hiyo huduma yenye mfumo wa end-to-end encryption.
6. Utajuaje iwapo ujumbe/call yako imewekewa ulinzi?
WhatsApp inakupa  uhuru wa kukagua iwapo ujumbe/call yako kwenda kwa mpokeaji vitakuwa vimelindwa.  Baada ya kutuma ujumbe wako kwa mpokeaji, iwapo mawasiliano yako na mpokeaji wako yatakuwa yamelindwa utapokea ujumbe huu “Messages that you send to this chat and cals are now secured with end-to-end encryption.” Kutokea hapo, unaweza kuona QR code ambazo ni namba ambazo ni tarakimu 60. Pia unaweza ku-scan QR code yako na kuhakiki kwa kuifananisha na zile tarakimu 60 za mtu unayewasiliana naye kwa wakati huo.
UJUMBE WENYEWE HUU HAPAmessages
7. Ni kwa namna gani WhatsApp wameweza kufanikisha hivi?
WhatsApp wametumia ‘The Signal Protocol’, iliyotengenezwa kwa Mfumo wa Open Whisper, kwa ajiri ya ulinzi wa kimtandao (encryption). Lengo lake ikiwa ni kuzuia watu wa kati (third paties) kuweza kuingilia mawasiliano hayo, mfano waharifu wa kimtandao (cybercriminals) na serikali ili wasiweze kuingilia mawasiliano binafsi.
8. Je, madhara yake ni nini kwa vyombo vya ulinzi?
Ulinzi huo utaleta changamoto kubwa kwenye vyombo vya usalama(polisi) na sheria (mahakama) kiduni hasa watakapotaka kuchunguza taarifa za matukio ya mtandaoni. Vyombo vya usalama pamoja na wizara yenye dhamana ya mawasiliano kwenye nchi husika ndiyo watakuwa na jukumu la kuhakikisha mawasiliano ya wananchi wao yanakuwa yamelindwa kabla whuduma haijaruhusiwa nchini.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment