Watoto wakiwa kwenye harakati za kuomba.
Stori: Hamida Hassan na Mayasa Mariwata
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutangaza kuanza
kwa oparesheni ya kuwaondoa ombaomba mtaani, hali imezidi kuwa mbaya na
sasa ombaomba hao wamebuni mbinu mpya kujipatia pesa huku wakimpiga
chenga ya mwili kiongozi huyo.
Katika maelezo ya Makonda, ombaomba hao wanatakiwa kurudi makwao kwa
kutumia gharama zao kama walivyotumia pesa zao kuja jijini ambapo
alisisitiza kuwa, itakapofika Jumatatu (keshokutwa) zoezi la kuwaondoa
kwa nguvu litaanza.
…..Zoezi hilo likiendelea.
Kufuatia agizo hilo, gazeti hili juzi lilifanya zoezi la kuzunguka
kwenye maeneo yenye ombaombao wengi hasa sehemu za makutano ya barabara
kama vile Magomeni Mataa, Fire na Moroco na kubaini kuwa, watu hao
wamebadili staili ya kuomba.
Mmoja wa vijana wanaofanya biashara ya kuuza maji katika maeneo ya Fire-Kariakoo jijini Dar alisema:
“Sasa hivi wale wamama na wababa hawaonekani kabisa huku barabarani,
wanampiga chenga Makonda. Wanajificha na kuwatuma watoto wao kuja
kuomba, halafu mtoto akija kuomba anasema kabisa ametumwa na mama yake
ili wapate nauli ya kurudi kwao.
“Ndiyo maana huwezi kuwaona wazazi wa watoto wao kule pembeni mwa
barabara kama ilivyokuwa awali. Wanakuambia kabisa naomba hela nipate
nauli ya kurudi kwetu! Sasa kama una huruma utashindwa kutoa pesa?”
alihoji kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rashidi Omari.
Kwa nini watoto ndiyo wanaonekana?
Inaelezwa kuwa, sababu ya wazazi wa watoto ombaomba kujificha ni kukwepa kukamatwa kwani watoto wao hata wakikamatwa bila wazazi wao ni kazi bure.
Inaelezwa kuwa, sababu ya wazazi wa watoto ombaomba kujificha ni kukwepa kukamatwa kwani watoto wao hata wakikamatwa bila wazazi wao ni kazi bure.
“Unajua lengo la serikali ni kuwarudisha ombaomba wote kwao, sasa
wakiwakamata watoto tu bila wazazi wao, zoezi haliwezi kufanikiwa, ndiyo
maana unatakiwa kupatikana ushirikiano wa kutosha kuwabaini wazazi wa
watoto hao wanaowatuma kuomba ili mpango wa kuwarudisha makwao
ufanikiwe,” alisema Salim Jumbe, dereva wa daladala inayofanya safari
zake kati ya Posta na Makumbusho na kuongeza:
“Halafu hawa watoto hata hawaogopi magari, wanatembea katikati ya
barabara bila kohofia pikipiki na magari, ndiyo maana unasikia kila siku
wanagongwa lakini hawasikii, waondolewe kwa nguvu tu.”
Ni tatizo kubwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa ombaomba hao ni
tatizo kubwa jijini Dar kwani wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa kwa
wasafiri na hata watembea kwa miguu.
“Yaani kazi hii imeonekana kama ni halali sasa, kila kukicha wanazidi
kuongezeka na wengine usipowapa pesa wanakutukana, kukukwangulia gari
yako na hata kukutemea mate. Mbaya zaidi ukitoa pesa yako kwa kumuonea
huruma, kesho lazima aje tena barabarani, matokeo yake wananogewa.
“Mimi nadhani hili aliloanzisha Makonda liungwe mkono na watu wote,
kweli wana hali mbaya lakini naamini kuna maisha mengine wanaweza kuishi
kuliko haya ya kuja kuombaomba,” anaeleza mama Janeth wa Kinondoni.
-via GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment