TAMBWE Akinukisha Kwa PLUIJM, Mashabiki

Amissi Tambwe
Sweetbert Lukonge na Said Ally
KIWANGO cha chini ambacho amekionyesha uwanjani siku za hivi karibuni mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, juzi Jumatano kilimchonganisha kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo.

Tambwe mwenye mabao 18 katika Ligi Kuu Bara ameshindwa kufunga na hata kiwango chake kimeonekana kuwa cha chini.
Baada ya mechi hiyo dhidi ya Mwadui FC, mashabiki kadhaa walimtaka kocha kutompanga Tambwe katika mechi zijazo na nafasi yake ichukuliwe na Malimi Busungu kwa madai kuwa hivi sasa anawazingua.

Hata hivyo, Pluijm alichukizwa na kauli hizo na ndipo alipoanza kuzozozana nao mpaka askari walipoingilia kati na kumtaka kocha apande gari aondoke uwanjani hapo.

Pamoja na hivyo, katika mazungumzo ya awali na gazeti hili kabla ya tukio hilo, Pluijm alionyesha kusikitishwa na kiwango alichoonyesha Tambwe.
“Sijui ni kwanini ila nitakaa na washambuliaji wangu waniambie wana matatizo gani kwani siyo kawaida yao,” alisema Pluijm ambaye pia alisema haridhishwi na kiwango cha sasa cha mshambuliaji wake mwingine, Donald Ngoma.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment