Jana May 5 2016 shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza rasmi kuwa klabu ya Azam FC imenyang’anywa point tatu na magoli matatu kutokana na kumtumia Erasto Nyoni ambaye alikuwa na kadi tatu za njano, katika mchezo wa 156 wa Ligi Kuu uliokuwa unazihusisha timu za Azam FC dhidi ya Mbeya City.
Baada ya taarifa hizo kutoka Sports Extra ya Clouds FM ilizungumza na afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Azam FC Saad Kawemba na kueleza
“Kwa sasa tumewapatia hilo suala benchi la ufundi ili waweze kufuatilia
na kuona uhalisia wa hicho kinachozungumzwa halafu watatueleza kama ni
kweli kosa hilo limefanyika halafu tutajua nini cha kufanya”
Maamuzi ya TFF kuinyang’anya point tatu na magoli matatu Azam FC
yanatokana na Kanuni ya 37(4) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 inayoelekeza
kuwa mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano katika michezo mitatu
hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata wa timu yake.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment