Baada ya SIMBA Kumfungia Mechi 5, Imeripotiwa Kaamua Kujiunga na YANGA na Kuomba Jezi Namba 25

Baada ya uongozi wa klabu ya Simba April 20 2016 kutangaza kumfungia mechi tano mchezaji wao Hassan Kessy kwa sababu za kucheza faulo ambayo ilimpelekea kuoneshwa kadi nyekundu na kuigharimu timu, usiku wa May 5 2016 mtandao wa salehjembe umeripoti kuwa beki huyo yupo katika hatua za mwisho kusaini Yanga. 

Katika mahojiano na salehjembe Kessy na meneja wake Hassan Tippo ‘Zizzou’ wamekubali kuwa wamefanya mazungumzo na Yanga na wapo katika hatua za mwisho kusaini mkataba Ijumaa ya May 6 2016, lakini pia Kessy  anadaiwa kuomba apewe jezi namba 25 ambayo ilikuwa inatumiwa na Emmanuel Okwi wakati yupo Yanga. 
Hassan Kessy
Hassan Kessy anaripotiwa kukaribia kumaliza mkataba ndani ya klabu ya Simba, lakini amefungiwa mechi 5 na Simba baada ya kumchezea faulo inayodaiwa kuwa ni ya makusudi Christopher Edward katika mchezo kati ya Simba dhidi ya Toto Africans.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment