Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kampeni hiyo, Shubert Mwarabu amesema, endapo meno hayo yatauzwa yatachochea ujangili kwani itaibuka imani miongoni mwa watu kuwa meno hayo yana soko na faida.
"Taiwan na China ambao ni miongoni mwa wateja wakubwa wa meno hayo wamefunga biashara hiyo kwenye masoko ya ndani hivyo haina sababu kutafuta wateja bali yachomwe," alisema.
Mwarabu amesema ili kuthibitisha kuwa biashara hiyo ni haramu, serikali haina budi kuonesha mfano wa wazi kwa kuteketeza meno hayo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment