Ushauri kwa TCRA Kuhusu zoezi la Kusitisha Matumizi ya Simu Bandia

TCRA wametoa taarifa kwa umma miezi michache iliyopita juu ya kusudio la Mamlaka hiyo kusitisha matumizi ya simu bandia ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Ni hatua nzuri na ya kupongeza lakini kwa bahati mbaya,kwa mtazamo wangu,naona imetolewa tu kama "briefing" pasipo kuwa na msisitizo wa kutosha pengine kwasababu mwezi June bado ni mbali kitu ambacho si sahihi.

Ushauri:
Viongozi wa Mamlaka,ikiwa imebaki takribani miezi mitatu kutekeleza zoezi hili,nawashauri muongeze utoaji wa elimu na taarifa kwa umma juu ya zoezi hili na pia mtoe tahadhari kwa umma kuacha kuendelea kununua simu hizi bandia maana bila shaka bado ziko sokoni na huenda nyingine ziko kwenye meli zinakuja.

Cha kufanya:
Mamlaka kwa kushirikiana na makampuni ya simu,mnaweza mkaanda ujumbe mfupi wa maneno(sms) kuhusu zoezi hili ambao kila mtumiaji wa simu atalazimika kuupata ujumbe huo kwanza kabla hajaweza kuongeza salio kwenye simu yake au kabla ya kupata salio la simu yake pale mtumiaji atakapotaka kupata huduma hizo.

Pia,ujumbe huu ambao pia utamuelekeza mteja namna ya kugundua kama simu yake ni bandia au laa,unaweza pia kuja kama ujumbe wa awali pale mteja atakapotaka kutumia huduma za m-pesa,tigo pesa,airtel money,n.k.

Njia nyingine ni kuanzia sasa kutumia vyombo vya habari kueneza ujumbe huu na zaidi kutahadharisha umma kuacha kuendelea kununua simu hizi za bandia na pia ikibidi mshirikiane na Shirika la Viwango Nchini(TBS) kufanya ukaguzi wa kushitukiza katika maduka mbalimbali ya simu na kuchukua hatua kwa watakaokuwa wanaendelea kuuza simu hizi za bandia ila mjue nanyi hapa hamtakwepa lawama kwa kuacha simu hizi ziingizwe nchini.

Sababu za ushauri huu:
Muda uliobaki ni mchache na jambo hili linaonekana kutopewa uzito wa kutosha licha ya athari kubwa za kiuchumi na kijamii zitakazokuja kujitokeza hapo baadae endapo zoezi hili litatekelezwa kwa muda uliopangwa.

Ni wazi simu za bandia zilizoko katika matumizi ni nyingi kuliko simu original lakini ndio hizi hizi zinazotumika katika shughuli za kibiashara,kiuchumi na kijamii.

Kwa mfano,ukisitisha matumizi ya simu bandia,ni wazi utaathiri kwa kiasi kikubwa wale waliojiajiri kwa kufungua vibanda vya m-pesa,tigo pesa, n.k.

Hatari nyingine iwapo umma utakuwa kama umeshitukizwa katika utekelezaji wa zoezi hili,itakuwa ni kupanda kwa ghafla kwa bei za simu original due to sudden increase in demand baada ya simu bandia kuzuiwa.

Kwa mtazamo wangu,hapa patakuwa na athari ya ziada ambapo watu wengi kushindwa kumudu bei za simu original ambazo kwa kawaida huwa ziko juu ukiachilia mbali ongezeko la bei litakolotokana na ongezeka la mahitaji ya bidha hiyo(increase in demand).

Athari nyingine itakayotokana na kupanda kwa bei ni kuwafanya watu wengi washindwe kununua simu hizi kwa uharaka kufidia pengo litakalokuwa limejitokeza na hivyo kuchukua muda mrefu zaidi kwa hali kurejea katika hali ya kawaida.

Mbali na sababu hizo,TCRA kwa kuanza kutoa elimu hii mapema na kuhamasisha umma juu ya zoezi hili ,itakuwa imejivua lawama kwa kutimiza wajibu wake mapema kabisa maana watanzania wengi hungoja dakika za majeruhi kutekeleza wanayopaswa kuyafanya na hili kila mtu ni shahidi na tuna mifano mingi tu kama vile watu kujiandikisha dakika za mwisho kwenye daftari la mpiga kura,n.k.
Ni mtazamo na ni ushauri pia.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment