Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo
ya uchaguzi ya Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa
mgombea wa jimbo hilo, David Kafulila inatarajia kutoa hukumu Mei 17,
mwaka huu.
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora anayesikiliza kesi hiyo mjini Kigoma,
Ferdinand Wambali alisema baada ya pande zote kuwasilisha ushahidi na
maelezo yao mahakamani hapo amepanga kutoa hukumu tarehe hiyo.
Kutolewa
kwa tarehe hiyo ya hukumu kunatokana na kufungwa kwa utoaji ushahidi wa
maelezo ya kesi hiyo ambayo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa
uchaguzi wa jimbo hilo, aliwa mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo.
Baada
ya kukamilika kwa ushahidi wa pande zote, Jaji Wambali ameomba kupatiwa
muda wa kutosha kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa
mahakamani hapo ili atoe hukumu ya haki.
Katika
kesi hiyo Namba Mbili ya mwaka 2015, David Kafulila aliyekuwa mgombea
ubunge wa jimbo hilo anaitaka mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi
mgombea wa CCM, Hasna Mwilima na badala yake mahakama imtangaze yeye
(Kafulila) kama mshindi halali wa uchaguzi katika jimbo hilo.
Walalamikiwa
katika kesi hiyo ni Mwilima, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali aliyeiwakilisha Tume ya Taifa ya uchaguzi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment