Jackson Mayanja ‘Mia Mia’
Nicodemus Jonas na Wilbert Molandi
KUONDOLEWA kwenye michuano ya Kombe la FA pamoja na ushindi wa Yanga, juzi dhidi ya Mwadui FC, kumempa nguvu Kocha wa Simba, Jackson Mayanja ‘Mia Mia’ ambaye ametangaza vita katika mbio za Ligi Kuu Bara.

Mayanja ameliambia Championi Ijumaa kuwa awali mipango na akili yote
ilikuwa kwenye mataji mawili lakini sasa vita iliyobakia ni kufa au
kupona kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa ligi kuu ili wapate nafasi ya
kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.
“Tulikuwa na karata mbili awali, lakini sasa tumebakiza moja. Ni
lazima tupigane, akili na mipango yetu yote imebakia sehemu moja (ligi
kuu) na kuhakikisha tunaendeleza wimbi la ushindi na kupambana mpaka
mwisho wa ligi, kitakachotokea ni hichohicho.
“Ni kweli mbio za ubingwa zimekuwa ngumu kwa sasa, lakini cha msingi ni sisi kuhakikisha tunakuwa makini zaidi pamoja na kupata sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki, viongozi na kila mmoja atimize wajibu wake,” alisema Mayanja.

Juuko atibua mahesabu yake
Aidha, Mayanja ambaye timu yake itacheza na Toto, keshokutwa itamkosa beki wa kati, Juuko Murshid ambaye ana kadi tatu za njano.
Aidha, Mayanja ambaye timu yake itacheza na Toto, keshokutwa itamkosa beki wa kati, Juuko Murshid ambaye ana kadi tatu za njano.
Mayanja alisema wachezaji wengine watakaoukosa mchezo huo ni Mwinyi
Kazimoto, Brian Majwega ambao wote ni wagonjwa huku kipa Vincent Angban
na kiungo Justice Majabvi wakiwa kwenye hatihati ya kutocheza kutokana
na kukosa mazoezi ya jana kwenye Uwanja wa Ndege Beach, Mbweni.
“Kumkosa Juuko ni pengo lakini hakuna jinsi, tutaangalia wengine
waliopo,” alisema kocha huyo wa zamani wa Vipers na Kagera Sugar.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment