Pep Guardiola Kamuomba Msamaha Cristiano RONALDO, Kisa?

Siku moja baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kuweka wazi kuwa angependa Real Madrid icheze na Benfica hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kauli hiyo aliitoa kabla ya mchezo wa marudiano wa Benfica na FC Bayern Munich kuchezwa.

Usiku wa April 13 2016 FC Bayern Munich ilicheza dhidi Benfica ya Ureno na kufanikiwa kuiondoa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya goli 3-2, hivyo ndoto ya Ronaldo ya kutamani Real Madrid icheze na Benfica ikawa imeishia hapo.

Baada ya FC Bayern Munich kufuzu hatua ya nusu fainali kwa kuitoa Benfica, kocha wa FC Bayern Pep Guardiola amemuomba Cristiano Ronaldo msamaha kwa kuikatisha ndoto yake ya kutamani Real Madrid icheza na Benfica nusu fainali, Guardiola aliongea katika lugha ya utani baada ya kuitoa Benfica.
“Samahani kwa kuivunja ndoto ya Ronaldo najua alipenda kucheza dhidi ya Benfica hatua inayofuata lakini haikuwezekana” >>> Guardiola
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment