Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania
nchini Japan.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa
Chikawe umeanza tarehe 13 Aprili, 2016.
Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Mheshimiwa Mathias Meinrad
Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo tarehe 15 Februari, 2016.
Mheshimiwa Chikawe aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nachingwea kati ya
Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika Serikali ya awamu ya
nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment