Ummy ameitaka MSD kuandika maelezo ya kina kwa
maandishi, kuhusu vifaa vya Sh2 bilioni ambavyo viko njiani kwenda
Muhimbili kwa miaka minne sasa, kabla wizara yake haijatoa tamko rasmi.
Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu jana alisema bohari
haina mzigo wowote ulio njiani kuelekea Muhimbili bali imekuwa
ikisambaza dawa zake nchi nzima.
Bwanakunu alisema tatizo
lililojitokeza ni mfumo wa kompyuta ambao unaonyesha mzigo upo njiani,
hivyo muamala katika kompyuta unavyoshindwa kukamilika, mzigo lazima
uonekane upo njiani.
“Mwaka 2012 tulibadilisha mfumo wa kompyuta
kutoka wa awali mpaka tunaotumia sasa, hivyo kuna miamala ilihitaji
kubadilishwa, mwaka huu tulifanya zoezi la kukamilisha baadhi na si kwa
Muhimbili pekee kwa mfano kuna mzigo unatoka MSD Ubungo kwenda Muleba ukifika kule mtu anashindwa kuingiza kwenye mfumo kwamba
umepokelewa,” alisema Bwanakunu.
Alifafanua kwamba majibu ya MSD
kwa CAG yalieleza kuwa walitengeneza timu ya uchunguzi na baadhi ya watu
walichukuliwa hatua, “nimeshachukua hatua za haraka baada ya kupata
hiyo ripoti, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wale ambao hawakujaza hiyo
miamala tulishawachukulia hatua, hakuna mali iliyopotea MSD.”
Taarifa
zaidi zinaeleza kwamba kuna ripoti ya Muhimbili ambayo inaonyesha katika
vitabu kwamba kuna mzigo ambao Muhimbili iliununua kutoka MSD, lakini
haujafika, lakini Bwanakunu alipoulizwa alisema hakuna vitabu
vinavyoonyesha kuwa Muhimbili inadai vifaa tiba na dawa MSD.
Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru
alisema kwa taarifa alizonazo mpaka sasa CAG alifanya ukaguzi katika
vitabu vya MSD na si wao na alipouliza vifaa viko wapi alijibiwa kuwa
vinakwenda MNH.
Alisema kuwa Watanzania wawe na subira na kwamba
watapewa majibu kesho (leo), baada ya Muhimbili kupekua kwa kina vitabu
vya mwaka 2012, ili kujiridhisha iwapo vifaa vilipokelewa au havikuwahi
kununuliwa Muhimbili.
“Hiyo ripoti tumeiona leo Jumanne. Hayo mambo
yametokea mwaka 2012 huwezi kuwa na jibu la kila kitu, kesho tunataka
tukapitie hiyo ripoti kwa sababu ni ukaguzi wa MSD, tukaangalie vitabu
hivyo vifaa vilifika?” Alisema Museru.
Naye Waziri Ummy Mwalimu
alisema katika ripoti hiyo kuna hoja mbili ambazo ni MSD na TFDA, huku
akifafanua kwamba amezungumza na Mkurugenzi wa MSD lakini hajaridhika na
majibu na kumtaka aandike maelezo ya kina.
“Nimetaka maelezo ya
maandishi kutoka kwa MSD na TFDA kuhusu ripoti ya CAG tumekubaliana na
Katibu Mkuu walete maandishi ndiyo tutatoa msimamo rasmi wa wizara, kwa
upande wa MSD ndiyo maana tuliweka pembeni wale wakurugenzi wanne sababu
ya changamoto hii ambayo CAG amekutana nayo,” alisema Ummy.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment