Usijikute Tu Umenunua Gari Kwa Dalali Jijini Dar


Leo April 15 2016 Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amekaa kwenye Exclusive interview kuelezea utapeli ambao unawapata watu wa Dar es salaam bila kuushtukia mchezo.

Kamanda Sirro anasema ‘Kumejitokeza watu wanatapeliwa na wizi wa magari, mtu anakwenda kijiweni anakuta gari ananunua, salali ni mtu aliyepewa kibali na mahakama, hawa wa vijiweni hawatambuliki‘

‘Watanzania wengi wanaangalia gari lenye bei ndogo, unajikuta unanunua gari ambalo ni la wizi na mwisho wa siku unabeba mzigo ambao siyo wako‘ ;-Kamanda Sirro
“Natoa wito kwa watu kwamba hawana sababu kununua magari kwa madalali, waende kwenye maduka ya kuuza magari, kwasababu imekuwa tatizo ” ;-Kamanda Sirro
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment