Kiti
 cha Spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Sheria 
pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi 
aliyofanya bungeni, badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio 
pekee. 
Aidha, kimewataka wabunge kubadilika na kuacha tabia ya kuchukua posho za vikao vya Bunge bila kuzitolea jasho.
Kauli
 hiyo imekuja kutokana na Mwongozo ulioombwa Aprili 25, mwaka huu na 
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ambaye alikitaka kiti cha 
Spika kutoa Mwongozo kuhusu usahihi wa wabunge wa Kambi Rasmi ya 
Upinzani Bungeni kulipwa posho na mishahara wakati hawashiriki na 
kutimiza wajibu wao wa kuchangia kwenye mjadala wa Bunge la Bajeti 
linaloendelea katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11.
Bashe
 alisema mbunge huyo alitumia Kanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu za 
Bunge akiomba Mwongozo wa Spika kutokana na Kambi Rasmi ya Upinzani 
Bungeni, kuamua kutoshiriki mjadala unaoendelea bungeni, lakini wabunge 
hao wanasaini na kulipwa mishahara na posho.
Hivyo akaomba Mwongozo endapo ni haki kwa wabunge hao kupokea posho wakati hawashiriki wala kutimiza wajibu wao wa kisheria. 
Katika kujenga hoja hiyo, Bashe alitumia Ibara ya 63(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isemayo, “Kwa
 madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza kujadili 
utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa 
bajeti.”
Aidha,
 Bashe alitumia Ibara ya 73 ya Katiba ya Tanzania kufafanua kuhusu 
malipo ya mshahara, posho na malipo mengine kwa wabunge. 
Akitoa
 Mwongozo wa Spika, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema kwa 
mujibu wa Katiba ya Tanzania, Ibara ya 73 imeainisha masharti ya kazi ya
 wabunge.
Alisema
 mbunge anastahili kulipwa mshahara kwa kila mwezi, na kufafanua kuwa 
mbunge anapohudhuria vikao bungeni na kamati atalipwa posho ya vikao kwa
 kiwango kitakachowekwa na Serikali na Kanuni za Bunge. 
Alisema malipo ya mshahara ni suala la Kikatiba na Sheria hulipwa kwa mbunge kutokana na kazi yake ya ubunge.
Hivyo
 malipo ya posho kwa wabunge yanatokana na mahudhurio yao bungeni na 
siyo kwa kuchangia kama ambavyo wengi wao wanapenda iwe hivyo. 
“Kimsingi
 kuhudhuria bungeni pekee siyo njia inayopendeza kwa kuwa mbunge 
anapofika bungeni anatarajiwa atekeleze majukumu yake yalivyoainishwa 
katika Ibara ya 63.
“…Tabia
 hii ya kutochangia mijadala na kuzunguka zunguka bungeni haikubaliki na
 haitakiwi kuendelea, kila mbunge atekeleze wajibu wake na sio 
anahudhuria ili alipwe posho,” alisema Dk Ackson.
Wakati
 huo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko katika Kamati 
mbalimbali za Bunge, kwa kubadilisha wabunge 16 wa Kamati za Awali 
kwenda nyingine. 
Aidha,
 Spika amewapangia Kamati wabunge wapya wanne, walioapishwa mwanzoni mwa
 Mkutano huu wa Bunge, ambao ni Shamsi Vuai Nahodha, Rita Kabati, Oliver
 Semuguruka na Lucy Owenya.
 TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]

0 comments:
Post a Comment