SERIKALI
imesitisha huduma za tiba asili zitolewazo na Kiliniki za Kikorea,
Maibong Sukidar Medical na Korea Medical Clinic zilizopo Jijini Dar es
Salaam kwa kosa la kutokuwa na kibali kwa zaidi ya miaka nane pia
kuchanganya tiba asili na za kisasa na mbadala bila ya idhini kutoka
baraza la usajili la tiba asili nchini
Hatua
ya kufungwa kwa kliniki hizo imechukuliwa jana baada ya Hamisi
Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto kufanya ziara ya kushtukiza kukagua vibali na huduma zitolewazo
katika kiliniki hizo.
Kigwangalla
alizitaja sababu zilizopelekea kufungwa kwa Kiliniki ya Korea Medical
kuwa ni pamoja na Kutibu magonjwa ambayo haikupewa kibali kutoka
serikalini na kuhifadhi dawa ambazo hazihusiani na magonjwa inayotibu
“Kliniki
hii ninaamuru ifungwe kwa makosa matano ikiwemo kosa la kuchanganya
tiba asili na kisasa, kutokuwa na kibali, usajili halali, matabibu wake
hawajui lugha ya Kiswahili na au kiingereza, usajili ulimtaka kuajiri
tabibu wa kitanzania ambaye hapa hayupo,” alisema Kigwangalla.
Alisema kliniki hiyo inatumia dawa kali za maumivu, usingizi, uzazi wa mpango, sindano na dripu.
Kigwangala alimwamuru msajili wa hospitali binafsi kufanya uchunguzi ili kubaini hizo dawa zilikuwa zinafanya kazi gani.
Aidha,
Kigwangalla alieleza sababu ya kufungwa Kliniki ya Maibong ni pamoja na
kutokuwa na kibali kwa zaidi ya miaka minane, kuchanganya tiba asili na
kisasa na kutoplekea vyeti vya matabibu wake kama serikali ilivyomtaka
kuvipeleka toka mwaka 2008.
“Kiliniki
hii haina kibali walichonionesha ni barua walizoandika za kuomba kibali
kutoka serikalini na kwamba serikali iliwaambia kupeleka vyeti vya
matabibu wake jambo ambalo hawajalifanya hadi sasa,” alisema.
“Baraza
la usajili tiba asili lifungie kliniki hadi itakaporekebisha nyaraka
zake pamoja na kufanyiwa uchunguzi kama inakidhi vigezo vya kutoa huduma
ya tiba asili na mbadala,” amesema.
Kigwangalla
alitoa agizo kwa baraza la usajiri la tiba asili nchini kuzifungia
kliniki hizo hadi zitakapofuata utaratibu, pia aliitaka idara ya
uhamiaji kuchunguza vibali vya makazi na ufanyaji kazi nchini.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment